KIUNGO wa Rwanda na Simba, Haruna Niyonzima, amesema moja ya malengo aliyojiwekea ni kuhakikisha timu hiyo inatwaa ubingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika hapo mwakani.Simba ilikata tiketi ya kushiriki michuano yaKombe la Shirikisho Afrika baada ya kuibuka mabingwa wa Kombe la FA msimu uliopita
Akizungumza nasi kiungo huyo
aliyejiunga na Simba msimu huu akitokea Yanga, alisema ubora wa kikosi chao ndio unaomfanya aamini wana kila sababu ya kubeba taji hilo.“Simba tuna kikosi bora msimu huu ndiyo maana nawaza ubingwa wa Afrika, naamini inawezekana kwa sababu ya aina ya wachezaji na kama tutajituma hakuna kitakachoshindikana,” alisema Niyonzima.
Niyonzima alisema licha ya ubora wa kikosicha Simba kwa sasa, anaamini yeye binafsi ana bahati ya kuzipa mafanikio timu mbalimbali alizowahi kuzichezea tangu akiwa nchini kwao Rwanda na baada ya kutua Tanzania.Alisema anatambua haitakuwa kazi rahisi, lakini kiu ya mafanikio waliyokuwa nayo msimu huu anaamini itawasaidia kufikia malengo.Hata hivyo, pamoja na kuichezea timu yake ya zamani ya Yanga kwa miaka mitano, Niyonzima hakuwahi kufanikiwa kutwaa ubingwa wowote wa michuano ya Caf.
No comments:
Post a Comment