Tshishimbi apewa tuzo/zawadi - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Wednesday 1 November 2017

Tshishimbi apewa tuzo/zawadi

Vicent Kigosi ‘Ray’ akikabidhi zawadi kwa wachezaji wa Yanga Ibrahim Ajibu, Papy Kabamba Tshishimbi na kipa Rostand Youthe.

KUNDI kubwa la mashabiki wa Yanga maarufu kama Yanga For Life, jana Jumanne lilitoa zawadi ya fedha na vifaa vya kuchezea mpira kwa wachezaji Ibrahim Ajibu, Papy Kabamba Tshishimbi na kipa Rostand Youthe.

Tukio hilo la makabidhiano lilifanyika Makao Makuu ya klabu hiyo yaliyopo mitaa ya Jangwani na Twiga jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Championi Jumatano, Vicent Kigosi ‘Ray’ ambaye ni mmoja wa viongozi wa kundi hilo alisema Ajibu amezawadiwa shilingi milioni moja baada ya kuchaguliwa mchezaji bora kwenye mechi mfululizo za Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar na Stand united.

Ray ambaye ni msanii wa Bongo Movie nchini alimtaja kiungo Tshishimbi kuwa ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mechi dhidi ya Simba na kuzawadiwa shilingi 500,000, viatu vya mpira ‘njumu’ na vikinga ugoko ‘shine guard’.

Aliongeza kuwa, kipa Mcameroon, Rostand Youthe amepewa shilingi 250, 000 na viatu vya mpira na vikinga ugoko kutokana na mchango alioutoa tangu aanze kuichezea timu hiyo.

No comments:

Post a Comment