Mbunge wa Jimbo la Ubungo Said Kubenea amesema kuwa ni uongo kuwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu hakupigwa risasi 30 kama inavyoelezwa bali Polisi walizihesabu na kukuta maganda 38 ya risasi kwenye gari lake.
”Lissu hakumiminiwa risasi 30 kama Spika alivyoliambia Bunge na Taifa, Lissu amemiminiwa risasi 38. Kwenye gari lake Polisi wameokota maganda 38 ya risasi.” – Alisema Saed Kubenea leo katika ibada ya Ijumapili kanisa la Ufufuo na uzima Ubungo leo Jijini Dar es salaam.
Kubenea amewasihi Watanzania kuzidi kuungana pamoja kwa kukemea na kulaani juu ya tukio hilo baya.
No comments:
Post a Comment