MABINGWA WA LIGI KUU BARA YANGA WAMEPANIA KUICHAKAZA NJOMBE MJI. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Thursday, 7 September 2017

MABINGWA WA LIGI KUU BARA YANGA WAMEPANIA KUICHAKAZA NJOMBE MJI.

Baada ya benchi la ufundu la timu hiyo kuwekea mkazo kwa safu ya ushambuliaji katika mazoezi yao.

Benchi la ufundi la timu hiyo lilikuwa likiwapa mazoezi maalum ya ufungaji washambuliaji , baada ya kuwasimamia kwa umakini zoezi hilo lililokuwa likiendelea uwanjani hapo.

Kocha Msaidizi wa Yanga, Shadrack Nsajigwa alisema, katika mechi yao ya kwanza walitengeneza nafasi nyingi, lakini walishindwa kufunga, hali iliyowafanya wafanyie kazi mapema.

"Tunafanyia kazi suala hili la ushambuliaji kwa sababu tulitengeneza nafasi nyingi kwenye mechi yetu ya kwanza, lakini hatukupata mabao ndio maana tumekazia hivi sasa,"alisema.

Yanga katika mchezo wake wa kwanza walitoka sare ya bila kufungana na Lipuli iliyopanda Daraja, licha ya kuwa walitengeneza nafasi nyingi.

No comments:

Post a Comment