LIVE: AZAM FC 0-0 SIMBA UWANJA WA CHAMAZI. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Saturday, 9 September 2017

LIVE: AZAM FC 0-0 SIMBA UWANJA WA CHAMAZI.

Dakika ya 13: Azam wanatengeneza nafasi mara kadhaa, mchezo unakuwa na kasi, timu zote zinapiga pasi ndefu.
Dakika ya 10: Nahodha wa Azam, Himid Mao anapewa kadi ya njano kwa kucheza faulo.

Dakika ya 7: Mchezo umeanza kwa kasi, ushindani upo sehemu ya katikati ya uwanja.

Dakika ya 5: Simba wanafanya shambulizi kali, mpira wa kichwa unaokolewa na kipa wa Azam FC inakuwa kona.
Dakika ya 2: John Bocco wa Simba anapuliziwa filimbi kwa kuunawa mpira, analalamika akidai mpira ulimgonga kifuani.

Mchezo umeshaanza dakika ya kwanza.
Timu zote zimeshaingia uwanjani, muda wowote mchezo utaanza.
Huu ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ambao utachezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex maarufu kwa jina la Uwanja wa Chamazi.

No comments:

Post a Comment