LISU AMEPELEKWA ICU, WACHEZAJI WAMETOA YA MOYONI. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Saturday 9 September 2017

LISU AMEPELEKWA ICU, WACHEZAJI WAMETOA YA MOYONI.

HALI ya Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu ambaye juzi Alhamisi alishambuliwa kwa risasi mjini Dodoma na watu wasiojulikana, imeelezwa amepelekwa chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) baada ya kufanyiwa upasuaji wa awali huko Nairobi, Kenya.

Lissu ambaye aliwahi kusema kuwa yeye ni shabiki wa Yanga wakati alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari na kudai tangu mwaka 1993 hajawahi kwenda uwanjani, alikumbwa na balaa hilo la kupigwa risasi tumboni na miguuni majira ya saa 7:00 mchana nyumbani kwake Area D baada ya kuegesha gari akitokea bungeni.

Kutokana ha tukio hilo, baadhi ya wachezaji wa zamani wa Simba na Yanga wameonyesha kusikitishwa vilivyo na kujikuta wakitoa yao ya moyoni.
Akizungumza kwa niaba ya wachezaji wa zamani wa Yanga, nahodha wa zamani wa timu hiyo, Sekilojo Chambua alisema: “Hakika tukio hilo limetusikitisha sana kwani siyo la kiungwana.

“Tuko hilo ambalo limetokea mchana kweupe kabisa hakika si jambo zuri hata kidogo, tunapaswa kulikemea vikali kwani mambo kama hayo siyo utamaduni wetu.”
Naye mchezaji wa zamani wa Simba, Boniface Pawasa, alisema: “Tukio hili limetuacha na maswali mengi juu ya watu hao ambao wamekuwa wakifanya matukio hayo na hawajulikani.

“Tunapaswa kukemea vikali matukio haya, tuwe na kampeni ya kukemea mambo kama haya kwa ajili ya kulinda heshima ya nchini yetu.”
Kwa mujibu wa Chadema, jana majira ya saa 10 alasiri, Lissu alitolewa ‘theatre’ alikokuwa anafanyiwa upasuaji wa saa saba akitolewa risasi.

Jana Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Vincent Mashinji, alilaani tukio hilo na kuitaka serikali kukomesha vitendo vya watu wasiojulikana kufanya matukio hatarishi

No comments:

Post a Comment