POLISI WAMEKAMATA MAGARI 8 TUKIO LA LISSU,WANAMSAKA DEREVA WAKE. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Saturday 9 September 2017

POLISI WAMEKAMATA MAGARI 8 TUKIO LA LISSU,WANAMSAKA DEREVA WAKE.

KAMANDA wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto amemtaka dereva wa Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema) Tundu Lissu, ajitokeze ili aweze kutoa maelezo yake kuhusiana na tukio la kupigwa risasi bosi wake.

Kamanda  huyo amesema kwamba sababu ya kumtafuta dereva huyo aliyemtaja kwa jina la Adam ni kwa sababu alikuwa pamoja na majeruhi wakati tukio hilo linatokea.

Pia Kamanda huyo alimtaka Katibu Mkuu wa Chadema Dk Vicent Mashinji kufika kwa RCO mjini Dar es Salaam ama Dodoma kutokana kauli yake kuwa katika uchunguzi wao wamewabaini wahusika.

Kamanda  Muroto amesema Polisi Mkoani Dodoma wamekamata magari nane aina ya Nissan Patrol kwa ajili ya uchunguzi wa tukio la kupigwa kwa risasi kwa mbunge wa Singida Mashariki (Chadema) Tundu Lissu.

Kamanda Muroto amesema uchunguzi huo unafanywa kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA).
“Uchunguzi wa awali umeonyesha kuwa wahalifu walikuwa na silaha ya SMG/SAR kutokana na maganda  ya risasi yaliyokutwa eneo,” amesema

No comments:

Post a Comment