KIPA WA MANCHESTER CITY ALIYE CHANIKA USONI AMERUDI MAZOEZINI - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Tuesday, 12 September 2017

KIPA WA MANCHESTER CITY ALIYE CHANIKA USONI AMERUDI MAZOEZINI

Kipa wa Manchester City, Ederson amerejea kwenye mazoezi lakini ameonyesha jinsi ambavyo alivyoumia usoni katika purukushani za kuwania mpira kati yake na mshambuliaji wa Liverpool, Sadio Mane.
Kipa huyo mwenye miaka 24 alitolewa uwanjani akiwa katika machela maalum baada ya kuumia usoni katika mchezo huo wa Jumamosi iliyopita.

Huu ni msimu wake wa kwanza akiwa City tangu aliposajiliwa kwa pauni milioni 35 akitokea Benfica ya Ureno.
Katika mazoezi ya jana alionekana akiwa amevaa kifaa maalum kuziba uso wake kwa pembeni ambapo alishonwa nyuzi kadhaa kutokana na kuchanika.

No comments:

Post a Comment