MSANII wa muziki kutoka Namibia , Betty G, amemtoa machozi Nandy kwenye Stage ya Coke Studio Africa baada ya kuimba wimbo wa Nandy na kuurudia wimbo huo wa One Day zaidi ya mara mbili na kuutendea haki kwenye jukwaa mbele yake.
Nandy ambaye ni mshiriki kutoka Tanzania kwenye msimu huu wa tano wa Coke Studio Africa , alishindwa kuzizuia hisia zake na kumwaga machozi ya furaha baada ya Betty G wa Namibia alipokuwa akiimbia kwa hisia kali na kuupatia ‘kinyama’ wimbo huo.
Haikuwa kwa Nandy tu, bali hadi kwa mashabiki waliokuwepo ndani nao walipagawishwa na mwimbaji huyo wa Namibia kwa kuwakonga nyoyo..
NA : ERICK PICSON
No comments:
Post a Comment