NIYONZIMA:TULIENI SIMBA HII BINGWA. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Monday, 25 September 2017

NIYONZIMA:TULIENI SIMBA HII BINGWA.

KIUNGO wa Simba, Mnyarwanda, Haruna Niyonzima, amewatuliza mashabiki wa timu hiyo, akidai licha ya matokeo ya sare waliyoyatoa dhidi ya Mbao, anaamini timu hiyo itatwaa ubingwa mwishoni mwa msimu.

Simba ambayo ina pointi nane katika msimamo wa ligi, imetoa sare michezo miwili na kushinda michezo miwili kati ya michezo minne iliyocheza.

Akizungumza Niyonzima amesema kuwa, kikosi chao kipo vizuri na wanaamini watafanikiwa kutwaa ubingwa licha ya upinzani mkubwa wanaokumbana nao.

“Kikosi cha Simba kwa ujumla kipo vizuri kwani hata mabao tuliyofungwa na Mbao yalikuwa ya kushtukiza, tulimiliki mpira kwa asilimia 90 ya mchezo na kilichotokea ni bahati tu ambayo haikuwa yetu.

“Kwa ubora wa kikosi chetu kilivyo, nina imani ya kuweza kutwaa ubingwa msimu huu, kikubwa zaidi ni kuweza kujituma uwanjani,” alisema Niyonzima.

No comments:

Post a Comment