SIKIA BUSARA ZA PAUL POGBA - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Monday 10 July 2017

SIKIA BUSARA ZA PAUL POGBA

Kiungo wa Manchester United, Paul Pogba.
PAUL Pogba bado anasubiriwa kuanza kufanya vitu vyake vilivyoifanya Manchester United ivunje rekodi ya dunia ili kumnasa msimu uliopita.
Katika maisha yake Manchester United, Pogba alipitia raha na karaha. Utakumbuka kuwa katika miezi ya hivi karibuni, Mfaransa huyo alimpoteza baba yake mzazi, mzee Fassou, akiwa na umri wa miaka 79. Pogba, 24, aliiongoza United kutwaa ubingwa wa Ligi ya Europa, siku mbili baada ya bomu lililodaiwa lilitokana na shambulio la kigaidi, kuua watu 22 jijini Manchester.
Tangu ajiunge Manchester United akitokea Juventus kwa ada ya rekodi ya dunia, Pogba amekuwa akifahamika kama mtu anayependa utani, anayependa kudansi na anayependa kuwa na staili mbalimbali za nywele. Anasema kuwa kifo cha baba yake wiki mbili kabla ya fainali ya Ligi ya Europa jijini Stockholm, Sweden, kilimkumbusha kuwa maisha yanatakiwa kufurahiwa.
Paul Pogba akiwa katika pozi baada ya mechi.
“Unapompoteza mtu unayempenda, huwezi kufikiri kwa namna ya kawaida. Ndiyo maana nasema ni lazima kufurahia maisha, kwa sababu yanakwenda kwa kasi sana.
Nakumbuka jinsi nilivyokuwa nazungumza na baba yangu na sasa hayupo. Alikuwa mtu imara sana, msumbufu vilevile. Alipambana (kuokoa maisha yake), lakini kwa umri wake haikuwa rahisi.
“Hapana, alikuwa mtu mzuri sana, baba mzuri sana na ninajivunia kuwa mwanaye. Alikuwa mmoja wa watu wacheshi sana, mcheshi sana. Kila wakati ukiwa naye ni lazima ucheke. Alikuwa na akili pia, kwa sababu alikuwa profesa. Ni lazima ukumbuke vitu vya furaha,” anasema Pogba.
Akizungumzia msimu wake wa kwanza United akiwa ni mchezaji ghali  z a i d i duniani, Pogba alisisitiza dau lake la pauni milioni 89, halikuathiri kiwango chake. “Baada ya wiki tu, nilisahau. Ni watu ndiyo walionikumbusha. Kwa sababu, mwisho wa siku, unapokufa, mtu wa thamani zaidi na asiye na thamani zaidi, wanakwenda kaburini. Kwa hiyo, hata sifikiri juu ya hilo.
” Pogba pia alijibu tuhuma za kiwango cha Manchester United msimu uliopita chini ya kocha Jose Mourinho huku akigusia makombe matatu waliyoyatwaa katika msimu wa kwanza wa kocha huyo Mreno. “Nakubali kwamba hatukucheza vizuri, hatukufanya hiki, hatukufanya kile. Najua tuilichokifanya — tulishinda m a k o m b e m a t a t u . Hicho ndicho ninachokijua. Na hilo ndilo suala la msingi. “Mnaweza kuwa timu bora duniani, mnaweza kucheza soka safi na mnakosa kombe lolote.
Na nani atakayewakumbuka? Hakuna. Sivyo?” United ilipata fidia ya pauni 800,000 ilipomuachia Pogba aondoke klabuni hapo kwenda Juventus ili kutafuta nafasi ya kucheza mwaka 2012. Anasema ni shauku ya kucheza mpira ndiyo iliyomfanya aondoke bila kukubaliwa na Sir Alex Ferguson — na anasema hakuwa akielewa matamshi ya bosi huyo wa zamani wa Manchester United wakati alipotua klabuni hapo kwa mara ya kwanza
akitokea Ufaransa akiwa na umri wa miaka 16. “Hapana! Hapana, sikuweza. Sikuwa hata nikiwaelewa wachezaji wenzangu na lafudhi zao.
Marafiki zangu sasa wananicheka. Wanasema, “Oh, nakumbuka siku za kwanza hukuweza kuongea, sasa unaongea kwa lafudhi kama zetu!” Inafurahisha sana. “Niliondoka Manchester ili nicheze. Hicho ndicho pekee nilichokitaka. Ingawa nilikuwa mdogo, nilihisi naweza kucheza na nisingeweza kusubiri. “Mama yangu aliniambia, “Utarudi tena siku moja”. Na sasa nipo: nanyoa nywele zangu Manchester.
” Pogba na rafiki yake wa karibu Mbelgiji, Romelu Lukaku, hivi sasa wapo Los Angeles, Marekani wakila bata kabla ya kuanza maandalizi ya msimu ujao, lakini kitu kizuri ni kwamba marafiki hawa wa nje ya uwanja, sasa wanaweza kupata nafasi ya kucheza pamoja katika kikosi cha Manchester United, kwani Lukaku anaelekea k u k a m i l i s h a uhamisho wake kutoka Everton kwenda Man U. Pogba na Lukaku wamekodi jumba la kifahari jijini Los Angeles wakifurahia maisha wakati huu wa mapumziko ya mwisho wa msimu.

No comments:

Post a Comment