IBRAHIM AJIB APIGA TIZI KWA MARA YA KWANZA YANGA. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Tuesday, 11 July 2017

IBRAHIM AJIB APIGA TIZI KWA MARA YA KWANZA YANGA.

Kuelekea msimu mpya wa 2017/ kikosi cha Yanga kimeanza mazoezi ya kujifua kwa ajili ya msimu huo ambapo wamekutana kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Kikosi hicho cha Yanga kimeanza mazoezi hayo chini ya Kocha Mkuu George Lwandamina lakini hakukuwa na mazoezi ya nguvu zaidi ilikuwa ni mazungumzo na kupasha misuli.
Kocha Lwandamina leo hakuwa bize kama ilivyozoelewa pindi anapokuwa mazoezini. Mshambuliaji Ibrahim Ajibu ambaye ametua kikosini hapo hivi karibuni akitokea Simba, alikuwepo na akafanya mazoezi mepesi pamoja na wenzake ikiwa ni mara yake ya kwanza kujumuika na wenzake.

No comments:

Post a Comment