MSUVA;ASANTENI SANA YANGA - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Friday, 28 July 2017

MSUVA;ASANTENI SANA YANGA

NDOTO ya kiungo mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva ya kwenda kucheza soka la kulipwa nje ya nchi ilitimia juzi Jumatano baada ya kiungo huyo kupaa hadi nchini Morocco kwa ajili ya kumalizana na Difaâ Hassani El Jadidi kabla ya kujiunga nayo rasmi.
Msuva anaikacha Yanga aliyodumu nayo kwa miaka mitano tangu alipoh a mia klabuni hapo akitokea Moro United mwaka 2012, baada y a kukamilika kwa dili hilo ambalo limesimamiwa na meneja wake, Jonas Tiboroha. Ndani ya klabu hiyo ya Difaa El Jadidi, Msuva ataungana na winga, Ramadhan Singano ‘Messi’ ambaye alishatangulia kujiunga na kikosi hicho akitokea Azam FC ambayo alimaliza mkataba.
Kiungo huyo anakuwa mchezaji wa saba wa Kitanzania kwenda kucheza soka la kulipwa nje ya nchi. Wengine ni Rashid Mandawa aliyepo Botswana, Elias Maguri anayecheza Oman, Thomas Ulimwengu (Sweden), Mbwana Samatta (Ubelgiji), Farid Mussa (Hispania) na Abdi Banda aliyejiunga na Baroka FC ya Afrika Kusini. M u d a mfupi kabla ya Msuva kukwea pipa kuelekea Morocco juzi Jumatano, Championi Ijumaa, lilipata nafasi ya kuzungumza naye na hapa anafunguka kama ifuatavyo:
Simon Msuva.
NINI UTAKACHOKIKUMBUKA NDANI YA YANGA?
“Daaah! Kuna vitu vingi sana nitavimisi baada ya kuondoka Yanga, siwezi kuvielezea sana lakini kikubwa ni juu ya utani ambao niliuzoea kutoka kwa wachezaji wenzangu, lakini hata kuzurura kwani nilishazoea nikitokea mazoezini naenda maskani ila huko Morocco sidhani kama nitafanya hivyo. “Nikiwa huko nitawakumbuka sana washikaji zangu ambao wamenifanya niwe hapa na wale ambao nimekaa na kushirikiana nao kwa kipindi chote nikiwa Yanga.
Hayo yalikuwa ni maneno ya simon msuva kwa watanzania.
Kwa habari zaidi na matukio ya picha mbalimbali tembelea ukurasa wangu wa Instagram @erickpicson.

No comments:

Post a Comment