Katika kile ambacho kinaonekana ni mwendelezo wa kuongeza chachu ya ushindani wa utaji wao wa jadi, Yanga imetupa dongo kwa wapinzani wao, Simba kuelekea kwenye msimu mpya wa 2017/18.
Kupitia ukurasa wa Instagram wa Yanga, wameweka video fupi inayomuonyesha nahodha wao akizungumza kuhusu wao kuweka kambi mkoani Morogoro.
Katika video hiyo, nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amesema anajua hali ya hewa ya Morogoro ni nzuri na wanaamini watamsikiliza vizuri mwalimu ili kupata maandalizi mazuri.
Cannavaro ameongeza kuwa Yanga ni timu ambayo imeshazoea kutwaa ubingwa, hivyo amewataka mashabiki kuendelea kuwaunga mkono katika wakati huu wa maandalizi kabla ya mchezo wao dhidi ya Simba, Agosti 23, mwaka huu.
Kauli hiyo ni kama dongo kwa Simba ambao hawajatwa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa misimu mitano mfululizo.
Kwa habari zaidi za matukio na picha ni follow Instagram @erickpicson .

No comments:
Post a Comment