MAHABA YA MCHEKESHAJI EBITOKE KWA BEN POL MPAKA KUJITUNZA USICHANA WAKE KWA AJILI YA BEN POL - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Saturday 10 June 2017

MAHABA YA MCHEKESHAJI EBITOKE KWA BEN POL MPAKA KUJITUNZA USICHANA WAKE KWA AJILI YA BEN POL

Mchekeshaji Ebitoke kutokea Timamu Africa Media kafunguka katika mitandao ya kijamii na vyombo vya habari kuhusu kumzimia mwanamuziki BenPol , Ebitoke amesema yeye kuanza kumpenda Ben Pol haja anza leo bali ni toka kitambo sana alimpenda ,lakini alikosa nafasi ya kueleza ya moyoni mwake kwa kipindi hicho kwani hakuwa akitambulika sana , kwa sasa kapata nafasi ya kueleza hisia za mapenzi kwa msanii Ben Pol kaitumia ipasavyo na kumuomba Ben Pol amuoe , kwa mara ya kwanza Ebitoke kutuma ujumbe wake kwa Ben Pol ili mpa matumaini makubwa sana na kusema Ben Pol hawezi akamkataa huyu mwanadada, sababu ya Ebitoke kuweka asilimia mia kwa Ben Pol kuwa hata mkataa ni majibu ya Ben Pol kwake kwani alimtumia comment ya i love you katika mtandao wa Instagram, kitu ambacho ni chakipekee kwa Ebitoke ni kuwa tayari kulea mtoto wa Ben Pol japo haja mzaa yeye na kaahidi kuwa makini sana kwa huyo mtoto zaidi ya hata mama yake mzazi aliye mzaa huyo mtoto , pia mwanadada Ebitoke amesema yupo tayari kwa lolote hata kuacha kazi yake ya uchekeshaji endapo Ben Pol hataipenda ila yeye yupo tayari kumpa ushirikiano Ben Pol katika kazi zake anazozifanya . Yalikuwa ni maneno ya mchekeshaji Ebitoke yenye mahaba ya dhati kwa Ben Pol , kama unavojua watanzania wengine wamesema Ebitoke anatafita kiki  ila yeye kakanusha kwani alipewa ruhusa na manager wake bila kipingamizi chochote , ndicho kimempelekea yeye kutangaza hisia zake hadharani , cha kufurahisha zaidi ni kwamba watu wengine wamekwisha fungua mitandao ya kijamii kama mtandao wa Instagram na kuupajina kama BEN POL_ EBITOKE na kuwa takia maisha mema Ebitoke na BenPol .  Kwa matukio ya picha nimekusogezea karibu yako .

No comments:

Post a Comment