DIAMOND PLATINUM NA ZARI KUTOLEANA MAPOVU MTANDAONI KWA MARA YA KWANZA - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Tuesday 13 June 2017

DIAMOND PLATINUM NA ZARI KUTOLEANA MAPOVU MTANDAONI KWA MARA YA KWANZA

Moja kati ya matukio yanayo tokea katika mitandao ya kijamii imefikia mpaka kwa Diamond Platinum na mpenzi wake Zari kutoleana mapovu katika mtandao wa instagram .Na hii ni baada ya Diamond Platinum kuweka picha ya Zari akiwa na mwanaume mwingine kwenye swimming pool na kuandika ujumbe unaosema , ndio maana wakati mwingine naonaga bora tu nile na kusepa maana hawathaminikagi wala kuaminika hawa , ni maneno ya Diamond Platinum katika picha aliyo weka katika mtandao wake wa Instagram. Lakini Zari hakuweza kukaa kimya bali alijibu kwamba ile picha yule mwanaume ni binamu yake marehemu Ivan aliyekuwa mume wake kwa zamani na kudai kwamba ile picha imepigwa na mwanamke wake huyo jamaa.
Kwa kujilinda yeye Zari kaongea kuwa wakati mwingine mwanamke anakuwa ni mtulivu ila watu wengine hutafuta sababu hasa za kujisafisha wao na kuonekana hawana makosa .
Huo ujumbe moja kwa moja ni kwa Diamond Platinum kuwa anataka kujisafisha yeye , Lakini la umuhimu zaidi ni kwamba hatutopenda kwa hawa wawili kuwa katika hizo tofauti bali waya malize.
Picha za tukio husika nimekuwekea karibu yako na zaidi ya picha nimekuaogezea hapa chini.

No comments:

Post a Comment