Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger.
KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger , amesema kuwa kila siku kiungo wake Jack Wilshere amekuwa akipambana kuona anarejea uwanjani kwa kasi.
Wilshere hajacheza mchezo wowote msimu huu kutokana na kusumbuliwa na majeraha ambayo aliyapata alipokuwa kwenye kikosi cha Bournemouth msimu uliopita kwa mkopo.
Jana mchezaji huyo alitarajiwa kurejea uwanjani kuichezea timu yake hivyo kwenye mchezo wa Kombe la Europa dhidi ya FC Cologne.
Kiungo Jack Wilshere
Huu utakuwa mchezaji wa kwanza kwa kiungo huyo kwenye kikosi cha Arsenal baada ya kupita miezi kumi na tatu.
“Jack amekuwa akipambana sana kuhakikisha kuwa anarejea kwenye hali yake ya kawaida, ni kati ya viungo bora sana.
“Nami sijawahi kukata tamaa juu yake, nimekuwa nikiamini kuwa atarejea uwanjani na kufanya mambo makubwa kuliko kipindi cha nyuma kwa kuwa huyo ni mchezaji bora,” alisema kocha Wenger.
Mchezo wa mwisho kwa Wilshere kuichezea Arsenal timu hiyo ilipata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Watford
No comments:
Post a Comment