KWA MARA YA KWANZA WOLPER KUWA HOST KATIKA SHOW YA HARMONIZE.. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Tuesday, 5 June 2018

KWA MARA YA KWANZA WOLPER KUWA HOST KATIKA SHOW YA HARMONIZE..

Kwa Mara ya Kwanza Mrembo Jackline Wolper Atakuwa Host katika Show ya Mpenzi wake wa Zamani Msanii anayetamba na Track Kali Kwa Sasa Mjini 'Kwangwaru' Yaani Harmonize
Akifunguka Hayo Muda Mfupi Uliopita Katika Press na Waandishi wa Habari, HarmoLove Amesema Kuwa Anakuja na Usiku wa KUSI (KUSI NIGHT) akishirikiana na Global Group na Katika Washereheshaji Watakaokuwa Juu ya Stage ni Pamoja na Wolper.

Ukiachana na Ex Girlfriend Kuwepo Katika Usiku Huo wa Kipekee, Harmo Atasindikizwa na Mpenzi wa Sasa Sarah Ambaye Amesema Ameanza Kumfundisha Kiitaliano na Anakijua Jua Kwa Sasa.

Aidha Star Huyo Kutokea WCB Amesema Kuwa Katika Wapenzi waliowahi Kutoka na Diamond Platnumz ikiwa atatakiwa achague wa Kuoa amesema Hawezi Chagua Kwa Sababu Utamu wa Mashemeji Zake Hao Haujui Ulivyo.

Show Hiyo Itafanyika Katika Ukumbi wa Dar Live Mbagala Tarehe 17 Mwezi Huu  Siku ya Alhamisi.

No comments:

Post a Comment