SHABIKI WA LIVERPOOL AJINYONGA.. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Sunday, 27 May 2018

SHABIKI WA LIVERPOOL AJINYONGA..

Mwanafunzi wa mwaka wa pili Chuo kikuu cha ‘St. Augustine’ kampasi ya Mbeya Moses Mashaka amejinyonga mara baadaya timu yake ya Liverpol kushindwa kutwaa ubingwa wa klabu bingwa barani ulaya.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Jijini Mbeya Naibu Kamishna wa Polisi  Mohamed Mpinga wakati akizungumza na eatv.tv ambapo amesema Moses (24) amejinyoka mara baadaya ‘kubet’ na timu yake kushindwa kutwaa ubingwa.
“Mwanafunzi wa chuo kikuu cha sauti mwaka wa pili anachukua shahada ya ualimu amefariki baada ya ‘kubet’ pesa ambazo hazijulikani ni kiasi gani na baadaya Liverpol kushindwa ndipo akachukua uamuzi huo”,amesema kamanda Mpinga
Aidha Kamanda Mpinga amewataka wanafunzi kuacha kutumia fedha za wazazi kwa mambo yasiyohusiana na masuala mazima ya elimu, kwani matokeo yake ni hasara kwa wazazi.

No comments:

Post a Comment