SITEGEMEI KUPATA PESA KUPITIA 'VIEWERS' : ALIKIBA - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Tuesday, 15 May 2018

SITEGEMEI KUPATA PESA KUPITIA 'VIEWERS' : ALIKIBA

Msanii wa BongoFleva mwenye 'hit song' ya 'Mvumo wa Radi' Alikiba maarufu kama King Kiba amefunguka na kudai yeye sio miongoni mwa wasanii wanaotegemea kupata pesa kutoka katika 'views' za Youtube kama baadhi yao wanavyofikilia vichwani mwao.
King Kiba ametoa kauli hiyo ikiwa zimepita siku kadhaa tokea video yake mpya ya 'Mvumo wa Radi' kushindwa kuendelea kuhesabu idadi ya watu walioitazama jambo ambalo wengi wao walidai kuna kuna mchezo anafanyiwa msanii huyo ili asiweze kufikisha views wengi kama ilivyokuwa kawaida yake kila atowapo video.
"Hii ndio mara ya kwanza kunitokea tatizo hilo ila halijaweza kuniathiri kwa namna yeyote ile. Ila nashukuru watu wamepata walichokuwa wanastahili nasio kwamba mimi nategemea pesa kutoka 'Youtube views', mimi nafanya muziki najua wapi napata pesa katika muziki wangu. Nilichokuwa nahitaji kiukweli ni mashabiki zangu waridhike na waelewe mimi ni msanii wa aina gani", amesema Alikiba.
Pamoja na hayo, Alikiba ameendelea kwa kusema "tunajua kwamba kuna hizi biashara za kuweka ma-robot katika 'Youtube' ili ionekane watu wana 'view' kwa wingi ila mimi binafsi ninaona ni utoto tu. Haitokuja kutokea hata siku moja kwamba Alikiba ameweka 'robot' ili apate 'views' nyingi, mimi nafanya muziki wangu kwa ajili ya watu na kwanini sasa nidanganye watu".
Wimbo wa Alikiba kwa sasa umetazamwa jumla ya watu milioni 1.2 na kushikilia nafasi ya kwanza katika ya video zilizotazamwa kwa kiasi kikubwa kutoka Youtube

No comments:

Post a Comment