Akizungumza Rammy amesema kiasi hiko cha pesa atahakikisha anakamkabidhi mwenyewe mtoto Sania, ambayo ni stahiki yake kutokana na kazi aliyoifanya marehemu mama yake kwenye filamu ya 'Hukumu' waliyoigiza.
“Kwanza nisingependa kutangaza rasmi kiasi ambacho kitamfikia kwa sababu sijui filamu mauzi yake yatakuwaje, lakini mimi kama Ramy Galis nitatoa kile ambacho Mungu atanibariki kupitia filamu hii, kutakuwa na asilimia kadhaa ambazo nitaziweka kwa niaba ya mtoto, na nitakaa chini na famlia ya mtoto wa pande zote mbili watakapokubaliana na sio nibaki nazo mimi, ni haki ya yule mtoto”, amesema Rammy Galis.
Sambamba na hilo Rammy Galis amesema filamu hiyo anakusudia kufanya uzinduzi wake mkoani Mbeya ambako Agness ametokea, na anasubiri msiba upite kabisa ili watu wasije wakasema amefuata kiki ya msiba kufanya kazi zake.
No comments:
Post a Comment