RAIS MAGUFULI AMTAJA ADUI WA WATANZANIA. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Saturday, 5 May 2018

RAIS MAGUFULI AMTAJA ADUI WA WATANZANIA.

Rais Dkt. John Magufuli amefunguka na kuwataka wananchi wa Tanzania watambue kwamba adui yao mkubwa ni maendeleo na wala sio vyama vya siasa kama baadhi yao wanavyofikilia kila uchao katika vichwa vyao na kupelekea kuanza kubiashana badala ya kuchapa kazi.
Dkt. Magufuli amesema hayo leo Mei 05, 2018 wakati msafara wake umesimamishwa na wananchi wa kijiji cha Mkula mkoani Morogoro na kueleza kero zao zinazowakabili ikiwemo ujenzi wa shule ya msingi yenye madarasa saba na hatimaye Rais Magufuli akaweza kuwachangia fedha taslimu Milioni 5 ili kuweza kuendelea na ujenzi huo.
"Mkazitumie hizo fedha vizuri kwa ajili ya maendeleo ya shule na mimi ntakuja kufuatilia, ole wenu mzitumie vibaya, mimi kutumbua huwa ipo pale pale. Nataka watoto wangu wanaosoma hapa ni wakute wanasoma vizuri", amesema Magufuli.
Pamoja na hayo, Rais Magufuli ameendelea kwa kusema "tunachohitaji sasa hivi ni maendeleo, mtabishana sana mtachelewa, adui yetu mkubwa ni maendeleo na wala sio vyama. Kwa hiyo tushikamane wote kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu, mimi ni mtumishi wenu, Rais wenu ni Rais wa watanzania wote. Tuchape kazi kwa ajili ya maendeleo yote. Lakini niwaombe Wabunge na Madiwani wenu wawe wa kwanza kufuatilia kero zenu".
Rais Dkt. John Magufuli bado anaendelea na ziara yake Mkoani Morogoro na leo hii anatarajiwa kuzindua daraja la Mto Kilombero lililopo wilayani Kilombero mkoani humo.

No comments:

Post a Comment