OMMY DIMPOZ : MIMI NA ALIKIBA KWA SASA HATUNA ULAZIMA - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Sunday, 6 May 2018

OMMY DIMPOZ : MIMI NA ALIKIBA KWA SASA HATUNA ULAZIMA

Msanii wa muziki wa bongo fleva ambaye anafanya vizuri na wimbo wake ‘Yanje’ Ommy Dimpoz ambaye ameshirikiana vyema na msanii kutoka Nigeria Seyi Shay amefunguka na kusema kuwa kwa sasa hakuwa na ulazima wa kufanya wimbo na Alikiba na kudai hata wangefanya pamoja inawezekana usingeshtua.
Ommy Dimpoz amesema hayo alipokuwa akipiga stori na kasema kuwa alifikiria kufanya kazi na msanii mwingine ili kuleta utofauti na kudai zipo kazi za Rock Star zitakuja ambapo atakuwa ameshirikiana na Alikiba. 
"Ingetokea wimbo huu ningefanya na Alikiba huenda kisingekuwa kitu cha ajabu sanaa, Alikiba yupo na mimi nipo na tunafanya kazi pamoja nyimbo zangu anazisikia zake pia nazisikia kwa hiyo tutakapohitaji kufanya kazi tunaweza kufanya ila kwa sasa hivi hatukuwa na ulazima kwa sababu mimi na yeye bado tunafanya mambo mengi kwa pamoja, hivyo zipo project kama za Rock Star hivyo nikaamua kufanya collabo zingine zingine maana muda si mrefu tumetoka kutoka Kajiandae na Alikiba

No comments:

Post a Comment