MIMI NI MSWAHILI HALISI : ALIKIBA - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Thursday, 17 May 2018

MIMI NI MSWAHILI HALISI : ALIKIBA

Msanii wa muziki nchini Alikiba amewataka watanzani pamoja na wasanii kujivunia kutumia lugha ya Kiswahili kwasababu ni lugha kubwa na watu wengi Duniani  hutamani kujifunza lugha ya Kiswahili.
Alikiba amesema hayo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari na amedai kuwa watanzania wanapaswa kujivunia kuitwa waswahili na wasione aibu na kuongeza kuwa hata katika nyimbo zake amekua akitumia kiswahili kama kuonesha jitihada za kuunga mkono lugha hiyo.
Lugha yetu ni nzuri lazima tujivunie, najivunia sana kuwa mswahili na kuongea Kiswahili na kutumia kiswahil katika kazi yangu ya kunipatia maisha, kwahiyo kila mtanzania ni lazima ajivunie kuwa mswahili, asikwambie mtu acha uswahili, ni lazima ujivunie sio sifa mbaya” amesema AlikibaAlikiba aliongeza kwamba hata akiwa anafanya matamasha nje ya nchi watu wengi wamekuwa wanataka kufundishwa lugha ya kiswahili kutokana na matamshi yake kuvutia.

No comments:

Post a Comment