MESSI ATWAA TUZO YA MCHEZAJI BORA. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Friday, 18 May 2018

MESSI ATWAA TUZO YA MCHEZAJI BORA.

Nyota wa Barcelona na Argentina Lionel Messi ameibuka mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa Ligi kuu ya soka ya Hispania (La Liga), kwa mwezi April.
Messi ambaye anaongoza kwa mabao kwenye ligi hiyo ametangazwa mshindi asubuhi hii na bodi ya La Liga. Katika mechi zake 4 alizocheza ndani ya mwezi April Messi ameifungia Barcelona mabao 6.
Ndani ya mwezi April Messi alifanikiwa kufunga 'hat-trick' mbili dhidi ya Leganes na Deportivo La Coruna ambazo zilimfanya kuongeza idadi ya mabao akimkimbia nyota wa Real Madrid Cristiano Ronaldo.
Ndani ya mwezi April, Baarcelona ilishinda 3-1 dhidi ya Leganes, 2-1 dhidi ya Valencia, sare ya 2-2 dhidi ya Celta Vigo na 4-2 dhidi ya Deportivo La Coruna, mechi ambayo iliwahakikishia kuwa mabingwa wa La Liga msimu wa huu.
Messi atakabidhiwa tuzo hiyo kwenye mechi ya Jumapili dhidi ya Real Sociedad kwenye uwanja wa Camp Nou. Mechi hiyo ni ya mwisho kwa La Liga msimu huu ambapo Barcelona watamuaga nahodha wao Andres Iniesta.

No comments:

Post a Comment