HABARI za chini ya kapeti zinaeleza kuwa mastaa wawili wasioshikika kwenye muziki, Wizkid na Tiwa Savage ni wapenzi.
Ishu nzima inaelezwa ilianza kwenye mitandao ya kijamii mara baada ya Wizkid kumuondoa ‘unfollow’ mzazi mwenzake ambapo kwa sasa amekuwa akifuatana na Tiwa kila kona.
Licha ya kuonekana mara kwa mara pamoja na kukumbatiana kwenye shoo, Tiwa akihojiwa juu ya hilo husema kuwa ni marafiki wa karibu tu.
“Kumpata mtu ambaye mtaaungana naye kwenye kazi ni sawa na kushinda bahati nasibu. Mwanamke shupavu huhitaji kushikwa mkono. Kuwa sawa kwa asilimia 100 kwa mtu anaye-kuzunguka ni kitu kizuri,” alisema Tiwa kwa kuzunguka ‘mbuyu’ mara baada ya kuulizwa kama anatoka na Wizkid.
Tiwa aliwahi kuwa katika uhusiano na Teel Billz na kubahatika kuzaa naye mtoto mmoja, Jamil.
No comments:
Post a Comment