MKONGWE wa filamu za Kibongo, Blandina Chagula ‘Johari’ amempa somo mwanamitindo matata Bongo, Hamisa Mobeto ambaye ni mzazi mwenza wa Mbongo-Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kwamba, awe makini kwani mapenzi ya mastaa yanaumiza na hayatabiriki.
Akizungumza Johari alisema, amewahi kuwa kwenye uhusiano na staa, lakini aliteseka na kupoteza muda hivyo angekuwa yeye ndiye Mobeto, asingerudi kwa Diamond, bali angeendelea na maisha mengine maana kurudi ni kuambulia maumivu tu, hakuna cha maana zaidi.
“Nimewahi kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na staa, uliniumiza sana na ndiyo maana nampa somo Mobeto kuwa makini sana ili kukwepa kuumiza moyo wake na kupoteza muda,” alisema Johari.
No comments:
Post a Comment