Msanii wa muziki Bongo, Ben Pol amefunguka kuhusu tetesi zinazodai kuwa rapper Darassa ametumbukia kwenye matumizi ya dawa ya kuelewa.
Muimbaji huyo anayetamba na ngoma ‘Zai’ ameiambia Clouds TV kuwa kitu hicho bado hakiamini kwani amekuwa akiwasiliana na Darassa mara kwa mara.
“Kusema kweli siamini, sina element yoyote inayonifanya niamini chochote kuhusiana na hizo tetesi kwa sababu ili mtu uweze kusema kitu lazima uwe na element ambazo umeziona lakini mimi hamna element,” amesema.
“Mimi tunaongea masaa mawili, saa zima kwenye simu, video call sometime kwa hiyo sioni kuna element ya hicho kitu,” ameongea.
Darassa amemshirikisha Ben Pol katika nyimbo mbili ambazo ni Sikati Tamaa na Muziki, huku Ben Pol akimshirikisha Darassa katika ngoma moja, Tatu.
No comments:
Post a Comment