NYASHINSKI AMEFUNGUKA SABABU YA KUTOFANYA KAZI NA WASANII WA WCB - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Friday 4 May 2018

NYASHINSKI AMEFUNGUKA SABABU YA KUTOFANYA KAZI NA WASANII WA WCB

Hit maker wa wimbo Malaika na nyimbo nyingine nyingi, Nyashinski amefunguka kuzungumzia kitu kinachokwamisha kufanya kazi na wasanii wa WCB.

Muimbaji huyo wa Kenya ambaye anafanya vizuri Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla, asema wasanii wa WCB wako busy sana ndio maana hajafanya kolabo yoyote na wasanii wa label hiyo ambao wanafanya vizuri kila kona ya Afrika.

“Ningependa sana kufanya kazi na wasanii wa Wasafi…lakini wako busy sana.” Nyashinski aliiambia BBC.

Nyashinski amesema anaamini wasanii wa label hiyo wanafanya vizuri kutokana na kufanya kazi kwa bidii hali ambayo inawafanya kuwa busy kutokana na shunguli mbalimbali za muziki wao.

No comments:

Post a Comment