Msanii wa muziki Bongo, Mimi Mars amesema baada ya kupunguza mwili wake kuna baadhi ya mashabiki wake hawakupendezwa na jambo hilo ila wanapaswa kusikiliza muziki wake na sio kujikita zaidi katika muonekano wake.
Mimi Mars amesema kuwa alilazimika kufanya hivyo ili kujiongezea kujiamini zaidi katika tasnia ya muziki na pia muonekano wa awali alikuwa hapendezwi nao.
Mimi Mars amesema kuwa alilazimika kufanya hivyo ili kujiongezea kujiamini zaidi katika tasnia ya muziki na pia muonekano wa awali alikuwa hapendezwi nao.
“Nilikuwa sijafurahi na nilichokuwa nakiona, ilikuwa inaninyima confidence kidogo, so ikabidi nijitengeneze, nibadilishe hilo suala kwa sababu confidence ni kitu ambacho kinahitajika sana hasa kwenye hii industry ambayo tupo,” Mimi Mars ameiambia Bongo5.
“Najua wengi hawajafurahia, hawajapenda, wamelalamika lakini is me, ninachokipenda mimi ndio kinanifaa mimi. Waendelee kuupenda muziki wangu na kuendelea kuusikiliza, mwili wangu waniachie mimi,” amesisitiza.
Muimbaji huyo anayetamba na ngoma ‘Papara’ ameongeza kuwa alitumia muda wa miezi minne hadi mitano kupata muonekano alionao kwa sasa kwa kubadilisha mfumo wa kula na kufanya mazoezi.
No comments:
Post a Comment