TID ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha eNewz kutoka EATV baada ya kupita takribani siku 24 tokea msanii huyo kutangaza wazi kuwa yupo katika mahusiano na mwanadada mmoja ambae alikuwa nae nchini Germany jambo ambalo wengi wao walitarajia kuoa ndoa ikifuata katika siku za usoni.
"Sijasema kama ninaoa mwezi wa sita (Juni) ila tulikuwa tunajifurahisha mimi na rafiki yangu usingizi katika 'comment' instagram ilikuwa utani tu sijafikilia kuwa hivyo. Unajua sasa hivi watu wanataka kutengenezea kama kiki kitendo cha kuoa, kwa hiyo mimi sio mtu kutafuta kiki kwa kutumia ndoa", amesema TID.
Mbali na hilo, TID hakusita kutoa siri za swahiba wake wa miaka mingi Q-Chief kwamba alishawahi kutangaza kutaka kuoa lakini mpaka sasa hakuna chochote alichokifanya.
No comments:
Post a Comment