Beki wa Madrid agundulika kuwa na tatizo la moyo ameondolewa kikosini kwa muda wa wiki 6. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Sunday, 1 October 2017

Beki wa Madrid agundulika kuwa na tatizo la moyo ameondolewa kikosini kwa muda wa wiki 6.

Ukisema ni taarifa za kushitua hautakuwa umekosea kama ambavyo beki wa kulia wa Real Madrid, Dani Carvajal alivyoshituka.

Ametakiwa kuwa nje ya uwanja kwa wiki sita baada ya kugundulika ana tatizo la moyo.

Hali hiyo ilisababisha Carvajal kuondolewa katika kikosi cha Madrid.

Taarifa zimeeleza beki huyo mwenye miaka 25 ameonyesha kushitushwa na hali hiyo lakini ametakiwa kuwa mtulivu na kuwaamini madaktari wakati wanalishughulikia tatizo lake.

No comments:

Post a Comment