TEGEMEA KUMUONA KIKWETE KWENYE NDOA YA ALIKIBA. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Saturday, 14 April 2018

TEGEMEA KUMUONA KIKWETE KWENYE NDOA YA ALIKIBA.

Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete amefunguka na kumshukuru msanii Alikiba kwa kumtembelea nyumbani Kwake Leo na kusema kuwa amempa taarifa kuwa ataoa hivi karibuni.

Kikwete amesema hayo leo April 14, 2018 kupitia mtandao wake wa twitter na kusema kuwa msanii huyo ambaye sasa bado anafanya vyema na wimbo wake wa 'Seduce me' amemwambia anatarajia kuoa siku za karibuni. 
"Namshukuru Alikiba kuja kunitembelea na kunitaarifu kuwa anatarajia kuoa hivi karibuni. Nimempatia nasaha zangu na kumtakia kila la kheri kwa jambo hilo jema aliloamua kufanya" alisema Kikwete 
Siku za karibuni kumekuwepo na taarifa kuwa Alikiba anatarajia kufunga ndoa na mlimbwende mmoja kutoka nchini Kenya ambapo taarifa zilikwenda mbali zaidi na kuonyesha maandalizi ya harusi hiyo yameanza kufanyika nyumbani kwa binti huyo huko nchini Kenya.

No comments:

Post a Comment