BASATA wameweka wazi kuwa katika mkutano hao ambao ulifanyika jana wamemtaka msanii huyo kwanza kuomba radhi Watanzania kwa kitendo hicho lakini pia baraza hilo limechukua jukumu la kuwakumbusha wasanii wengine juu ya matumizi ya mitandao ya kijamii na kuwataka kutumia mitandao ya jamii kwa lengo la kujiletea maendeleo.
"Baraza linawakumbusha na kuwaasa wasanii wote kutumia maendeleo ya teknolojia na mitandao ya kijamii kwa lengo la kujiletea maendeleo badala ya kutumia mitandao kusambaza vitu visivyo na manufaa kwao na vyenye kuwadhalilisha wao wenyewe, familia zao na umma kwa ujumla" alisema taarifa ya BASATA
Hata hivyo msanii Nandy jana alipotoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) aliweza kuandika maelezo marefu na kuomba radhi kwa Watanzania kwa kitendo cha video yake ya faragha kuvuja mtandaoni.
No comments:
Post a Comment