SIMBA YATEMBELEA NYOTA YA YANGA. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Wednesday 4 April 2018

SIMBA YATEMBELEA NYOTA YA YANGA.

Vinara wa Ligi kuu soka Tanzania Bara Simba SC , imerejea mkoani Iringa kwa ajili ya kuweka kambi na ikiwa na Siku moja tangu ipate ushindi dhidi ya Njombe mji kama ilivo kuwa kwa yanga baada ya kufungwa na Singida United ilirejea kuweka kambi Morogoro.

Katika taarifa yake leo Simba, imeeleza kuwa kikosi chote kimeanza safari asubuhi hii kutoka mkoani Njombe kuelekea mkoani Iringa ambapo kitaweka kambi ya muda kabla ya kwenda mkoani Morogoro. 
Simba iliweka kambi ya muda mkoani Iringa baada ya kutoka Dar es salaam na kisha kwenda Njombe ambako jana ilicheza mchezo wake wa raundi ya 21 na kushinda kwa 2-0 dhidi ya wenyeji Njombe Mji na leo imerejea tena Iringa.
Yanga nayo iliweka kambi mkoani Morogoro kabla ya kwenda Singida ambako ilifungwa na Singida United kwenye robo fainali ya kombe la shirikisho. Baada ya mchezo Yanga ilirejea Morogoro na kuweka kambi. 
Simba itasafiri kutoka Iringa kuelekea Morogoro siku ya Ijumaa tayari kwa mchezo unaofuata dhidi ya Mtibwa Sugar. Mchezo huo utapigwa April 9 kwenye uwanja wa Jamhuri Morogoro.

No comments:

Post a Comment