SERIKALI YAWAPA SIKU 23 WANANCHI WANAO MILIKI ARDHI BILA KULIPA KODI. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Friday, 6 April 2018

SERIKALI YAWAPA SIKU 23 WANANCHI WANAO MILIKI ARDHI BILA KULIPA KODI.

Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya makazi, William Lukuvi amesema serikali itafikisha mahakamani na kuwafutia hati ya umiliki wananchi wote wanao miliki Ardhi ambao hawalipi kodi ya Ardhi.

Lukuvi ametoa kauli hiyo mara baada ya kupokea taarifa mbalimbali kutoka kwa watendaji wake ambapo amesema serikali inapoteza mapato mengi kwa kuwa baadhi ya wananchi kukosa uaminifu wa kulipa kodi ya ardhi kwa wakati.
Kutokana na hali hiyo, Waziri Lukuvi amesema ameamua kutoa muda hadi Aprili 30, 2018 ili kila mtu anayemiliki ardhi awe amekwisha lipa kodi hiyo na kwa wale ambao hawatalipa kodi kwa wakati ni wazi serikali itawafikisha mahakamani, kuwafutia hati za viwanja hivyo na kuviuza upya kwa wamiliki wengine ama kuuza nyumba zao.
Aidha Mhe. Lukuvi amewataka wafanyakazi wa wizara hiyo kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika zoezi hilo ili kupunguza ukubwa wa kazi na kukusanya fedha kwa wakati na kuongeza pato la taifa.

No comments:

Post a Comment