"NAVUTIWA ZAIDI NA JOKATE KULIKO WEMA" : HAJI MANARA. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Thursday, 19 April 2018

"NAVUTIWA ZAIDI NA JOKATE KULIKO WEMA" : HAJI MANARA.

Mkuu wa habari na mawasiliano Simba ,Haji Manara amesema anavutiwa sana na mrembo Jokate Mwegelo kwa sababu ni mtu anaye penda kusikiliza na kupokea ushauri.

Akizungumza na kusema kwamba kati ya wanawake maarufu waliopo nchini anavutiwa zaidi na Jokate kuliko Wema Sepetu.
“Mimi ni mshabiki sana wa Jokate Mwegelo, nampenda sio kimapenzi niweke wazi ni rafiki yangu, kati ya wasichana maarufu, nampenda sana Jokate, inatokea tu hata Jokate akisemwa vibaya naumia, halafu anasikiliza ni aina ya mwanamke ambae hata kumshauri unasikia raha”, amesema Manara.
Manara amesema kuhusu kumuoa Wema Sepetu, ilikua ni utani ambao aliuweka kwa nia ya kusisitiza hoja yake kuhusu kubadilishwa kwa ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara
Sambamba na hayo Manara amekiri kwamba, Wema Sepetu, ni msichana mrembo na ni moja kati ya watu wenye nguvu na ushawawishi mkubwa na anaweza kutumika hata katika matukio makubwa ya nchi.

No comments:

Post a Comment