MREMBO WEMA SEPETU NI MWENDO WA KUOGA MAMILIONI TU.. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Sunday, 8 April 2018

MREMBO WEMA SEPETU NI MWENDO WA KUOGA MAMILIONI TU..

BAADA ya kupewa Tuzo ya Msanii Bora wa Kike 2018 zilizokuwa zikitolewa na Sinema Zetu International Film Festival (SZIFF) zilizofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar hivi karibuni, staa wa Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu, sasa anaoga mamilioni ya fedha.

Mara tu baada ya tukio hilo, bishosti huyo alijikuta akilamba dili nono la kusainishwa mkataba na kampuni mpya ya kusambaza filamu za Kibongo ya Agusta.

Akizungumza  juu ya suala la kuogelea kwenye mkwanja, Wema alisema kuwa, anaishukuru kampuni hiyo kwa kuchukua kazi yake ya Heaven Saint na kumlipa donge nono, jambo ambalo limemfanya kuzidi kukaza buti ili kuendelea kufanya kazi nzuri zaidi kwani pesa aliyolipwa ingekuwa ni ndoto kwenye makampuni mengine.
“Kwanza nina furaha sana kuchukua tuzo ambayo ninajua kabisa imenipa heshima ya kutosha. Kingine imeniwezesha kupata dili kubwa la pesa ambazo zinaniwezesha kucheza hata filamu tatu, jambo ambalo ninajivunia na kutembea kifua mbele kabisa,” alisema Wema kwa ile sauti yake ya kubana.

Uchunguzi wa Ijumaa Wikienda ulibaini kwamba, mbali na kulamba shilingi milioni mbili za ushindi wa tuzo mbili pale ukumbini, dili alilopata ni la zaidi ya shilingi milioni 35 kwa awamu ya kwanza pekee.

No comments:

Post a Comment