Monalisa amezungumza hayo wakati akikabidhiwa bendera ya Taifa na Waziri wa Habari, Michezo, Sanaa na Utamaduni, Mh. Harrison Mwakyembe ambapo amesema kuwa ingawa anaamini atarudi nchini na tuzo hizo lakini hata akizikosa ni moja ya ushindi kulingana na kuwania waigizaji anaoshindana nao.
“Tuzo hizi nazichukulia kama ni heshima kubwa sana kwangu kwani kipengele ninachowania kinahusisha wasanii wakubwa katika bara la afrika kwani niko pamoja na Lupita Nyong'o ambaye ni mwigizaji wa Hollywood pamoja na Jackie Apia ambaye naye anafanya vizuri hivyo. Hata nisipopata tuzo hii kwangu kuchaguliwa kwanza katika kipengele hicho tayari ni ushindi kulinga na uwezo wasanii wenzangu tuona shindana,” Monalisa.
Kwa upande wa Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu nchini Bi. Joyce Fissoo amesema anafurahishwa kuona sekta ya filamu ikikua na kuleta taswira mpya katika bara la Afrika ambapo wasanii wa Tanzania nao kazi zao zinavuka mipaka na kuleta changamoto katika ushindani wa tasnia ya filamu Afrika.
Monalisa anatarajiwa kwenda Ghana mapema wiki hii amabapo atawawakilisha wasanii watatu ndani ya tasnia ya filamu ambao ni King Majuto anayewania Tuzo ya Mchekeshaji Bora Afrika, Raymond Kigosi anayewania Tuzo ya msanii Bora wa Kiume Afrika na Monalisa mwenyewe anayewania Tuzo ya Msanii Bora wa Kike Afrika pamoja na Mpiga picha Mahiri Moiz Hussein anayewania Tuzo ya Mpiga Picha Bora Afrika.
No comments:
Post a Comment