VITA YA SARAH NA WOLPER KUGOMBANIA PENZI LA HARMONIZE YAANZA UPYA NI BALAA. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Monday, 9 April 2018

VITA YA SARAH NA WOLPER KUGOMBANIA PENZI LA HARMONIZE YAANZA UPYA NI BALAA.

MKALI wa Bongo Movies, Jacqueline Wolper Massawe na  mzungu ambaye ni mpenzi wa Staa wa Bongo fleva kutoka WCB Harmonize, Sarah wamerudi kwenye ya vita ya mtandaoni.

Wolper na Sarah wamerushiana maneno Kwenye mtandao wa Instagram ambapo Sarah amemtuhumu Wolper kwa kumtumia meseji za Siri Harmonize huku akijua wazi kabisa ni mpenzi wake.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Sarah ameandika maneno haya kumtolea povu Wolper na kumchana kuwa anamtongoza Harmonize na kumtumia meseji huku anaona wazi kuwa hamjibu na amemtaka Wolper aishi maisha yake.

Hii  sio mara ya kwanza kwa Wolper na Sarah kugombana kisa penzi la Harmonize, siku za nyuma Sarah ameshawahi kuanika kuwa Wolper bado anamtaka Harmonize jambo ambalo Wolper amekuwa akikataa siku zote.

No comments:

Post a Comment