KALIO LANGU KUBWA NDO LILILO NIPA MCHUMBA : AUNTY LULU - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Wednesday, 11 April 2018

KALIO LANGU KUBWA NDO LILILO NIPA MCHUMBA : AUNTY LULU

KATIKA hali ya kushangaza, mwanadada ambaye ni mtangazaji wa zamani wa runingani na msanii wa filamu za Kibongo, Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’ ameibuka na kueleza namna ambavyo kalio lake limempatia wachumba watatu wa Kichina.

Akistorisha na Za Motomoto News, Aunty Lulu alisema kuwa, katika safari yake ya kibiashara nchini China hivi karibuni, aliingia kwenye ukumbi ambako kulikuwa na shoo ya Mtanzania na alipofika huko alijikuta akianza kukata mauno na wanaume wa Kichina waliokuwemo humo walianza kumshobokea hivyo kupata wachumba watatu wanaotaka kumuoa.

 “Kalio langu limenipatia wachumba wa Kichina watatu, sasa baada ya wote kuniambia wanataka kunioa, niliwatajia mahari yangu kuwa ni shilingi milioni 50 na walikubali, lakini niliwapa mtihani mwingine kwamba atakayekuwa wa kwanza kufika Bongo ndiye atakayenioa, hivyo ninasubiri na ndoa yangu itakuwa ya mkataba,” alisema Aunty Lulu.

No comments:

Post a Comment