FAHAMU SIRI YA MSANII ALIKIBA KUFUNGA NDOA SIKU YA LEO - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Thursday, 19 April 2018

FAHAMU SIRI YA MSANII ALIKIBA KUFUNGA NDOA SIKU YA LEO

Unafahamu siri ya msanii Alikiba kufunga ndoa Siku ya Leo ? Basi unatakiwa kufahamu kuwa mtoto wa nyoka ni nyoka tu hawezi kuwa mjusi.

Sababu ya msanii huyo kufunga ndoa siku ya leo ni kutokana na kufuata nyayo za wazazi wake ambao walifunga ndoa siku kama ya leo miaka mingi iliyopita.
Hilo amelithibitisha Alikiba kupitia mtandao wake wa Instagram.
Kupitia mtandao huo Kiba ameandika, “Siku ya leo Ndio Siku Mama Yangu Na Baba Yangu walifunga Ndoa ALHAMDULILAH #KingKiba.”
Alikiba amefunga ndoa alfajiri ya leo (Alhamisi) ya April 19 huko mjini Mombasa nchini Kenya na mrembo Aminah Rekish Mohammed. Hata hivyo sherehe nyingine kubwa ya ndoa hiyo inatarajiwa kufanyika siku chache zijazo jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment