ZLATAN,MANCHESTER UNITED WAACHANA KIMTINDO. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Friday, 23 March 2018

ZLATAN,MANCHESTER UNITED WAACHANA KIMTINDO.

MANCHESTER, ENGLAND. Zlatan Ibrahimovic amekamilisha uhamisho wake wa kwendaLA Galaxy akionyesha picha yake pamoja naSimba.
Ibrahimovic anayejifananisha naSimba alitumavideoyake akiwa najezi yaGalaxy: "Los Angeles, karibu Zlatan."
Ibrahimovic naManchester United wameamua kuchana mkataba uliokuwepo baina yao nastaa huyo wa kimataifawa Swedenjana alitazamiwa kuendelea namaisha mengine kwa kujiunga naklabu yaLA Galaxy.
Dili laZlatan kwendaGalaxy linatazamiwa kuwa mkatabawa pauni 1milionikwa mwaka na lilitazamiwa kutangazwa kama tangazokatika ukurasamzima wa gazeti maarufu laMarekani, Los Angeles Times na alitazamiwa kwenda California kwa ajili ya kutambulishwa.
Zlatan mwenye umri wa miaka 36amesaini mkatabampaka mwishoni mwa msimuna anawezakucheza mechi yake ya kwanza kwa wababehao katika pambano la Ligi Kuu ya Marekani dhidi yawatani wao wa jadiLAFC Machi31.
United ilithibitisha jana kwamba walikuwa wameukomesha mkatabawa staahuyo ambayekwa mara ya kwanza sasa atacheza nje ya bara la Ulaya baada yakutamba katikaklabu za Barcelona, Ajax, Paris Saint-Germain, Juventus, Inter Milan na AC Milan.
Zlatan mwenyewe aliandika katikamtandao wake akisema “Mambo mazuri ufika mwisho nahuu ni wakati wa kuendelea namaisha mengine baada ya kuwa namisimu mizuri miwili naManchester United.”
“Asante sana kwa klabu, mashabiki, timu, kocha na wafanyakazi wengine ambao walishirkiana namimikatika sehemu hii ya historiayangu.:”
Zlatan alikuwa akihusishwa kwa muda mrefu kujiunga na klabu hiyo ambayo iliwahi kuwachukua David Beckham na Steven Gerrard katikanyakati mbalimbali na sasa Zlatan anakwenda kufungua ukurasa mpya klabuni hapo.

No comments:

Post a Comment