DAVINA KUTUMIKIA UTAPELI.. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Friday, 23 March 2018

DAVINA KUTUMIKIA UTAPELI..

STAA wa filamu za Kibongo, Halima Yahaya ‘Davina’ amejikuta anaingia kwenye kashfa ya utapeli baada ya mtu ambaye hajafahamika kutumia jina lake kutapeli watu kupitia Mtandao wa Facebook.

Akizungumza Davina alisema hakuna kitu kinachomnyima raha kama mtu kutumia jina lake kwa mambo ya kitapeli kwani watu wasiojua wanamchukia wakidhani ni yeye, kitu ambacho hajawahi kufanya hata siku moja.

“Kitendo cha mtu huyo kutumia jina langu halafu anaomba hela kwa watu kinanisikitisha na kunitia doa kwani tabia hiyo mimi sijawahi kuifanya, nawaomba watu wawe makini katika hilo maana huyo ni tapeli mkubwa anayetumia vibaya majina ya mastaa,” alisema Davina.

Baadhi ya watu wasio waaminifu wamekuwa wakitumia majina ya mastaa kutapeli watu mitandaoni na hata Jackline Wolper aliwahi kukutwa na janga hilo hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment