YANGA YAONGEZA SILAHA MOROGORO - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Wednesday, 28 March 2018

YANGA YAONGEZA SILAHA MOROGORO

Nyota wanne wa kikosi cha mabingwa wa soka nchini Yanga,wanatarajia kusafiri mchana huu kutoka jijini Dar es salaam kwenda Morogoro kwa ajili ya kuungana na wenzao katika kambi ya timu hiyo.

Wachezaji hao ni Kelvin Yondani, Ibrahim Ajib, Hassan Kessy na Gadiel Michael, ambao wote walikuwa na timu ya taifa Taifa Stars iliyocheza mchezo za kirafiki Machi 22 dhidi ya Algeria na jana Machi 27 dhidi ya DR Congo.
Aidha taarifa ya klabu hiyo imeeleza kuwa golikipa namba mbili wa timu hiyo Ramadhani Kabwili ambaye naye alikuwa na timu ya taifa hatasafiri bali anabaki Dar es salaam kwaaajili ya majukumu ya timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 20 Ngorongoro Heroes.
Yanga imeweka kambi mkoani Morogoro ikijiandaa na mchezo wake wa robo fainali ya kombe la shirikisho (ASFC) dhidi ya Singida United. Mchezo huo utapigwa April 1 kwenye dimba la Namfua mjini Singida.

No comments:

Post a Comment