ZARI ALAMBA SHAVU KWENYE KAMPUNI YA BONGO,AGOMA KUMZUNGUMZIA DIAMOND - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Wednesday, 28 March 2018

ZARI ALAMBA SHAVU KWENYE KAMPUNI YA BONGO,AGOMA KUMZUNGUMZIA DIAMOND

MPENZI wa zamani wa mwanamuziki Diamond Platnumz, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ leo amesaini mkataba na kuwa balozi wa Kampuni ya Kedz Tanzania inayojishughulisha na utengenezaji wa Pampas.

Hafla ya kusainiana mkataba huo imefanyika kwenye Hoteli ya New Africa jinini Dar es Salaam ambapo Zari amesema anashukuru kupata mkataba na kampuni hiyo.

Alipoulizwa na wanahabari uhusiano wake na Diamond uliovunjika, alikwepa swali hilo akidai kuwa si kilichomleta. “Unajua hii ni kazi na haihusiani kabisa na masuala ya familia, hivyo nisingependa kulizungumzia hilo leo,”alifafanua.

Zari ambaye amezaa watoto wawili na Diamond, Februari 14, 2018 alitangaza kuvunja uhusiano na msanii huyo  na baadaye alipohojiwa na BBC Swahili, Zari alisema ameamua kuachana na Diamond kutokana na sababu mbalimbali moja ikiwa ni kushikana hadharani na mwigizaji Wema Sepetu.

No comments:

Post a Comment