SITEGEMEI MPENZI WANGU KUPAKA MAKE-UP : NIKI WA PILI - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Wednesday, 21 March 2018

SITEGEMEI MPENZI WANGU KUPAKA MAKE-UP : NIKI WA PILI

Msanii kutoka kampuni ya Weusi, Nikki wa Pili amesema uzuri wa msichana au mwanamke unatoka na asili yake aliyozaliwa nayo na wala haitokani na vitu vya kujiremba na kudai haitokuja kutokea mke wake kuonekana amejiremba kwa kuwa anataka awe 'natural'

Nikki wa Pili ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha eNewz kutoka EATV baada ya kupita siku kadhaa tokea msanii mwenzake Dogo Janja ku-comment katika ukurasa wake kwa kumwambia vitu 'natural' aviachie misitu na kumtaka aache ubahili wake amtunze mke wake wa kumrembesha na urembo.

"Sisi binadamu wenye ni wazuri kwasababu ni asili kwahiyo hakuna uzuri wowote duniani unaoweza kuzidi asili. Ninachoamini mimi ni kwamba uzuri wa msichana upo katika asili yangu", amesema Nikki wa Pili

Pamoja na hayo, Nikki wa Pili ameendelea kwa kusema "mimi ni mtu creative kwa hiyo siamini kwenye 'material' ninaamini kwenye nguvu ya ubunifu, kwenye kazi yangu naekeza kwenye ubunifu so labda watu wanatafsiri hivyo lakini ubunifu unanguvu mara elfu. Mimi napenda asili kwa hiyo sitegemei kumuona mpenzi wangu akiwa amejipaka make-up".

No comments:

Post a Comment