SINA MPANGO WA KUWAPA KIKI NISHA NA BROWN.. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Tuesday, 27 March 2018

SINA MPANGO WA KUWAPA KIKI NISHA NA BROWN..

Muigizaji wa Bongo movie na mfanyabiashara maarufu Jacqueline Wolper ameibuka na kuweka wazi hana mpango wa kuwapa kiki Nisha na Brown walioanika penzi lao hivi karibuni.

Wiki iliyopita msanii Salma Jabu ‘Nisha’ alianika Hadharani Penzi lake na Ex boyfriend wa Wolper anayejulikana kama Brown jambo lililowashangaza watu wengi hasa kwa sababu ya urafiki wa Wolper na Nisha.

Gazeti la Ijumaa Wikienda linaripoti kuwa Nisha na Brown walianza kunyemeleana tangu Brown akiwa na Wolper Lakini pia inasemekana wawili hao walikuwa wanawasiliana kwa siri siri Jambo lililosababisha migogoro na Wolper.

Baada ya stori hizi kutrend sana Wolper alitafutwa ili kutaka kujua kama alikuwa ana taarifa kuwa alinyakuliwa na Nisha:

"Jamani mimi sijui lolote, niko bize na cherehani yangu na mambo mengine hayanihusu kabisa lakini Sasa hivi sitoi kiki kwa mtu yoyote, niko bize na mambo yangu, mimi mambo ya watu hayanihusu kabisa”.

Nisha na Brown wamekuwa waki posti video na picha Kwenye mitandao ya kijamii kuonyeshana mahaba na hata Brown kafuta tatoo ya Wolper Kifuani kwake na kumuweka Nisha.

No comments:

Post a Comment