KUNA uwezekano mkubwa kwa Paul Pogba kuihama Manchester United mwishoni mwa msimu huu huku timu za Italia zikipewa nafasi kubwa ya kumsajili.
Uhusiano wa Pogba na kocha wake, Jose Mourinho sio mzuri na staa huyo amejikuta akisotea benchi mara nyingi katika siku za karibuni.
Taarifa zaidi zinaeleza kuwa Pogba amechoshwa na hali hiyo na angependa kurudi kwenye soka la Italia.
Uvumi uliopo ni kuwa Juventus inafuatilia hali yake kwa sasa na AC Milan nayo pia inasikilizia hatma yake.
No comments:
Post a Comment