JIKE SHUPA AVUNJIWA MLANGO KISA HIKI HAPA - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Tuesday, 20 March 2018

JIKE SHUPA AVUNJIWA MLANGO KISA HIKI HAPA

UBUYU wa wiki hii ni wa embe, ukiumung’unya, lazima mwishoni ukutane na ugwadu! Ubuyu wenyewe unamhusu muuza nyago aliyepata umaarufu kupitia video ya Wimbo wa Jike Shupa, Zena Abdalah ‘Jike Shupa’.

Mwanadada huyu asiyeishiwa vimbwanga amejikuta kwenye fedheha kubwa baada ya kuvunjiwa mlango wake na ndugu zake kwa madai hawataki akae na wanaume tata (mashoga) nyumbani kwake, Mwananyamala-Ujiji jijini Dar wiki iliyopita.

UBUYU KAMILI
Mtoa ubuyu wetu ambaye ni ndugu wa Jike Shupa aliyeomba hifadhi ya jina ili asionekane ‘kirusi’ aliliambia Ijumaa Wikienda kuwa, muuza nyago huyo siku zote anapenda kuishi na kutembea mitaani na wanaume hao, jambo ambalo lilisababisha baadhi ya ndugu kugoma kufika nyumbani kwake.

“Unajua ndugu wengi wa Jike Shupa wamegoma kufika nyumbani kwake kwa sababu marafiki zake karibia wote ni wanaume tata, jambo ambalo hawalifurahii kabisa,” kilimwaga ubuyu chanzo hicho.

NDUGU WAMFUNGIA KAZI
Msambaza ubuyu huyo alinyetisha kwamba, baadhi ya ndugu zake walijipanga na kumfungia kazi nyumbani kwake ambapo walifika hapo majira ya saa moja usiku.

MLANGO WAVUNJWA
Chanzo kilitiririka kwamba, baada ya baadhi ya ndugu hao kufika nyumbani hapo, walikuta mlango umefungwa, walipogonga, Jike Shupa aliwachungulia na alipowaona, akagoma kufungua mlango.

“Baada ya kugoma kufungua mlango wakati walishahakikishiwa kuwa yupo ndani ndipo kikaibuka kimbembe cha hatari kwani walikuwa na jazba na ukizingatia ni familia iliyoshika sana Dini ya Kiislam.

WAFUNGA MTAA
“Kilichofuata ni kuanza kusukuma mlango kwa nguvu hadi wakauvunja. Hawakuamini macho yao
maana walikutana na hao wanaume tata waliokuwa wamejilaza ndani kisha wakawatoa kwa kuwazaba vibao. Ishu hiyo ilijaza umati na kufunga mtaa,” kilipenyeza ubuyu chanzo hicho.


IJUMAA WIKIENDA NA JIKE SHUPA
Kama ilivyo desturi ya Ijumaa Wikienda, baada ya shuhuda huyo kuweka nukta, lilimtafuta Jike Shupa na kumweka mtukati ambapo mambo yalikuwa hivi;
Ijumaa Wikienda: Vipi tena Jike Shupa, nini kimetokea hadi ukavunjiwa mlango?
Jike Shupa: Mh! Hiyo habari mmeipata wapi?

Ijumaa Wikienda: Siku hizi hakuna siri, kama ulificha, basi sasa mambo hadharani hivyo wewe funguka tu!

Jike Shupa: Ila mbona hiyo ishu imeshaisha? Ilikuwa ni ndugu zangu tu…
Ijumaa Wikienda: Ndugu zako wamefanya nini hadi wakakuvunjia mlango?

Jike Shupa: Si kwa ajili ya ndugu zangu hawa (wanaume tata). Wanasema hawapendi nikae nao, lakini mimi naona ni kama watu wengine tu jamani.

Ijumaa Wikienda: Kwa hiyo bado unakaa nao?
Jike Shupa: Hapana…sasa hivi wako makwao, wanakuja tu kunisalimia na kuondoka.

Ijumaa Wikienda: Poa, asante Jike Shupa kwa ushirikiano wako.

Jike Shupa: Poa.

No comments:

Post a Comment